المؤمنون
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَمْ لَمْ يَعْرِفُوا۟ رَسُولَهُمْ فَهُمْ لَهُۥ مُنكِرُونَ ٦٩
{69} Na kauli yake Mwenyezi Mungu, "Au hawakumjua Mtume wao,ndiyo maana wanamkataa?" Yaani, au walizuilika kufuata haki kwa kuwa mtume wao Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - hakuwa maarufu kwao, basi wakawa wanamkanusha wakisema, 'Hatumjui yeye wala hatujui ukweli wake, ametulingania [mpaka] tuitafiti hali yake na tuulize kumhusu yeye kwa yule aliye na habari juu yake?' Yaani, haikuwa hivyo; hakika wao walimjua kabisa Mtume - rehema na amani za Mungu ziwe juu yake, - mdogo kwa mkubwa, wanajua kutoka kwake kila tabia nzuri, na wanajua ukweli wake na uaminifu wake, mpaka wakawa wanamwita - kabla ya utume. - Al-Amin (Mwaminifu); basi kwa nini hawakumsadikisha alipowajia na haki kubwa na ukweli ulio wazi?