انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المؤمنون
السورة ٢٣

المؤمنون

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦١

أُو۟لَـٰٓئِكَ يُسَـٰرِعُونَ فِى ٱلْخَيْرَٰتِ وَهُمْ لَهَا سَـٰبِقُونَ ٦١

{61} "Basi wote hao ndio wanaokimbilia katika mambo ya heri," na hamu yao kubwa ni yale yatakayowaleta karibu na Mwenyezi Mungu, na utashi wao umeelekea tu kwenye yale yatayowaokoa kutokana na adhabu yake. Kwa hivyo, kila jema wanalolisikia au wakapata fursa [kulifikia], wanaichukua fursa hiyo na kuharakisha kulitekeleza. Waliwatazama vipenzi wa Mwenyezi Mungu na wateule wake mbele yao, kulianini kwao na kushoto kwao; wanakimbilia kufanya kila jambo la heri, na wanashindana katika kutafuta kuwa karibu na Mola wao Mlezi. Kwa hivyo, wakashindana nao. Na kwa vile yule anayeshindana na mwenzake anayekwenda mbio, huenda akatangulia kwa bidii yake na kujiandaa kwake vyema, au huenda asitangulie kwa sababu ya kutofanya kwake hilo vyema, Yeye Mtukufu akajulisha kwamba, hawa pia ni miongoni mwa kundi la watakaotangulia. Akasema, "Na ndio," kwa ajili ya mema "watakaotangulia kuyafikia," na wamekwisha fika kilele chake, na wakashindana wao na kizazi cha kwanza. Na pamoja na haya, tayari walikwisha pata kutoka kwa Mwenyezi Mungu, utangulizi wa furaha kwamba wao ndio watakaotangulia.