انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المؤمنون
السورة ٢٣

المؤمنون

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٥

إِنْ هُوَ إِلَّا رَجُلٌۢ بِهِۦ جِنَّةٌ فَتَرَبَّصُوا۟ بِهِۦ حَتَّىٰ حِينٍ ٢٥

{25} "Huyu si lolote isipokuwa ni mwanamume mwenye wazimu. Basi mngojeeni tu kwa muda," mpaka kifo kitakapomfikia. Na hizi fikira potofu [ambazo] walizitumia ili kupinga unabii wa nabii wao, zinaonyesha ukubwa wa ukafiri wao na ukaidi wao, na kwamba wao ni wajinga sana na wapotofu wa mwisho. Kwa maana, hizo hazifai kutumiwa kupinga kwa njia yoyote ile, kama tulivyotaja. Bali hizo zenyewe zinaangushana na kukinzana. Kwa hivyo, kauli yake, "Huyu si chochote isipokuwa ni mtu tu kama nyinyi. Anataka kujipa ubora juu yenu." Walithibitisha kwamba ana akili anayowadanganya kwayo ili awashinde na awe bwana juu yao, na anahitaji pamoja na hayo kutahadhariwa ili wasidanganyike naye. Basi inawezaje kauli hii kupatanishwa na kauli yao, "Huyu si lolote isipokuwa ni mwanamume mwenye wazimu?" Je, hili si isipokuwa kutoka kwa mfananishaji, mpotofu, aliyegeukiwa na mambo, ambaye nia yake ni kuzuia haki kwa njia yoyote ile anayokubaliana nayo, ambaye hajui anachosema? Naye Mwenyezi Mungu anakataa isipokuwa kudhihirisha hizaya ya mwenye kumfanyia uadui na kuwafanyia uadui Mitume wake.