الحج
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْحَقُّ وَأَنَّهُۥ يُحْىِ ٱلْمَوْتَىٰ وَأَنَّهُۥ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ ٦ وَأَنَّ ٱلسَّاعَةَ ءَاتِيَةٌ لَّا رَيْبَ فِيهَا وَأَنَّ ٱللَّهَ يَبْعَثُ مَن فِى ٱلْقُبُورِ ٧
{6 - 7} Vielelezo hivi viwili vya ushahidi vinaashiria matakwa haya matano, nayo ni haya: "Hayo ni:" yule aliyemuumba mwanadamu kutokana na alivyowabainishia na akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, "kwa sababu hakika Mwenyezi Mungu ndiye Haki." Yaani, Mola Mlezi anayeabudiwa, ambaye hapana mola apasaye kuabudiwa isipokuwa Yeye, na kumuabudu Yeye ni kweli, na kumuabudu asiyekuwa Yeye ni batili. "Na kwamba hakika Yeye ndiye mwenye kuhuisha wafu:" kama alivyoanza kuumba, na kama alivyoihuisha ardhi baada ya kufa kwake, "na kwamba hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu." Nguvu na ukubwa wa uumbaji wake, "Na kwamba hakika Saa (ya Qiyama) itakuja hapana shaka kwa hilo" na hapana msingi wa kuizuia. "Na kwamba hakika Mwenyezi Mungu atawafufua walio makaburini," ili waweze kulipwa kwa matendo yao mema na mabaya.