الأنبياء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَنُوحًا إِذْ نَادَىٰ مِن قَبْلُ فَٱسْتَجَبْنَا لَهُۥ فَنَجَّيْنَـٰهُ وَأَهْلَهُۥ مِنَ ٱلْكَرْبِ ٱلْعَظِيمِ ٧٦ وَنَصَرْنَـٰهُ مِنَ ٱلْقَوْمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَآ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَوْمَ سَوْءٍ فَأَغْرَقْنَـٰهُمْ أَجْمَعِينَ ٧٧
{76-77} Yaani: Na mkumbuke mja wetu na Mtume wetu Nuh, amani ziwe juu yake, akimsifu Mwenyezi Mungu alipomtuma kwa watu wake, na akakaa nao miaka elfu kasoro miaka hamsini. Anawalingania kumwabudu Mungu, na anawakataza wasimshirikishe, na anajitokeza na kurudia rudia baina yao, na anawaita kwa siri na kwa sauti kubwa, mchana na usiku, lakini alipowaona, mawaidha hayakuwa na manufaa kwao, na karipio lilikuwa halina faida kwao. Akamwomba Mola wake Mlezi na akasema: "Mola wangu Mlezi! Usiachie katika ardhi makazi ya makafiri. "Hakika ukiwaacha watawapoteza waja wako, wala wao hawatazaa ila waovu makafiri." Basi Mwenyezi Mungu akamjibu na akawazamisha na hakuacha hai hata mmoja wao, Mwenyezi Mungu akamuokoa Nuhu na familia yake na Waumini pamoja naye katika safina iliyosheheni, na akawafanya dhuria wake kuwa ndio waliobakia, na Mwenyezi Mungu akampa ushindi juu ya watu wake waliomdhihaki.