الأنبياء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُلْ إِنَّمَآ أُنذِرُكُم بِٱلْوَحْىِ ۚ وَلَا يَسْمَعُ ٱلصُّمُّ ٱلدُّعَآءَ إِذَا مَا يُنذَرُونَ ٤٥
{45} Yaani, "Sema:" Ewe Muhammad, kwa watu wote: Sema: Mimi nakuonyeni kwa Wahyi;" yaani, mimi si vinginevyo isipokuwa ni mjumbe, sijawaletea jambo lolote kutoka kwangu, wala sina hazina za Mwenyezi Mungu, sijui yaliyofichika, wala sisemi kwamba mimi ni malaika, isipokuwa mimi nawaonya kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu amenifunulia. Ikiwa mtakubali, mtakubali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, naye atawalipa kwa hilo, na ikiwa mtakengeuka na kupinga, sina amri yoyote katika jambo hilo, lakini amri ya jambo hilo iko kwa Mwenyezi Mungu, na makadirio yote ni ya Mungu. "Wala viziwi hawasikii wito;" yaani, viziwi hawasikii sauti, kwa sababu masikio yao yameharibiwa na hayafanyi kazi, na sharti ya kusikia pamoja na sauti ni kupatikana mahali panapofaa jambo hilo. Vivyo hivyo, ufunuo ni sababu ya maisha ya mioyo na roho na kwa ajili ya kufahamu kuhusu Mwenyezi Mungu. Lakini ikiwa moyo hauwezi kusikia mwongozo, utakuwa (moyo huo) kwa niaba ya uwongofu na imani upo katika tabaka ya kiziwi kwa niaba ya kuskia sauti. Kwa hivyo hawa washirikina ni viziwi kwa niaba ya mwongozo; kwa hivyo haishangazi kwa kukosa kwao kuongoka, haswa katika hali ya kutojiliwa na adhabu, wala hayajawagusa maumivu yake.