انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنبياء
السورة ٢١

الأنبياء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٤٢

قُلْ مَن يَكْلَؤُكُم بِٱلَّيْلِ وَٱلنَّهَارِ مِنَ ٱلرَّحْمَـٰنِ ۗ بَلْ هُمْ عَن ذِكْرِ رَبِّهِم مُّعْرِضُونَ ٤٢

{42} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, akitaja unyonge wa wale walioshika miungu isiyokuwa Yeye, na kwamba wao ni wahitaji sana kwa Mola wao Mlezi, Mwingi wa Rehema, ambaye rehema zake zinajumuisha watu wema na wasiomcha Mungu katika usiku na mchana wao. Na akasema. "Sema: Nani anayewalinda?" Yaani, anayewachungana kuwahifadhi "usiku" mnapolala juu ya vitanda vyenu na hisia zenu zimepotea? Na wakati wa mchana ni wakati wa kujishughulisha na kughafilika kutokana "na Arrahmani Mwingi wa Rehema;" yaani, badala yake na kitu kingine. Yaani, je, kuna yeyote anayekulinda isipokuwa yeye? Hakuna mlinzi ila yeye. "Bali wao wanapuuza kumkumbuka Mola wao Mlezi:" Ndiyo maana waliungana naye, vinginevyo; na lau wangerejea kwa Mola wao Mlezi, na wakapata mawaidha yake; wangeongoka kwenye njia yao iliyonyooka, na wangefaulu katika mambo yao.