الأنبياء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَقَالُوا۟ ٱتَّخَذَ ٱلرَّحْمَـٰنُ وَلَدًا ۗ سُبْحَـٰنَهُۥ ۚ بَلْ عِبَادٌ مُّكْرَمُونَ ٢٦
{26} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya upumbavu wa washirikina wanaomkadhibisha Mtume, na kwamba walidai - naye akawakemea - kuwa Mwenyezi Mungu alijichukulia mwana. Na wakasema: Malaika ni binti za Mwenyezi Mungu! Mwenyezi Mungu ametukuka mbali na maneno yao hayo, na akawajulisha kuhusu maelezo ya Malaika kwamba wao ni waja waliolelewa na kuendeshwa, na hawana lao jambo katika mambo hayo. Na wao wametukuzwa tu kwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu aliwalazimisha na akawafanya kuwa katika waja wake watukufu na wanaorehemewa. Na hilo ni kwa sababu ya fadhila mahususi alizowapa na kuwatakasa kutokana na machafu, na kwamba wao ni wenye adabu kubwa sana mbele ya Mwenyezi Mungu na wanatekeleza amri zake.