انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنبياء
السورة ٢١

الأنبياء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٣

لَا يُسْـَٔلُ عَمَّا يَفْعَلُ وَهُمْ يُسْـَٔلُونَ ٢٣

{23} "Yeye haulizwi kwa ayatendayo" kwa sababu ya ukuu wake, na uwezo wake kamili, hakuna yeyote anayeweza kumzuia wala kumpinga, siyo kwa maneno wala kwa vitendo. Na ukamilifu wa hekima yake na kuweka kwake vitu katika mahali pake, na ustadi wake ndicho kitu kizuri zaidi ambacho akili inaheshimu. Kwa hivyo haulizwi swali lolote, kwa sababu uumbaji wake hauna kasoro yoyote wala dosari. "Na wao" yaani, viumbe vyote, "ndio wanaoulizwa" juu ya vitendo vyao na maneno yao; kwa sababu ya kutoweza kwao na umaskini wao, na kwa kuwa ni waja. Na hawana uwezo uzito wa chembe wa kutenda na kujiendesha wao wenyewe wala wengine.