انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · طه
السورة ٢٠

طه

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٩–١٠

وَهَلْ أَتَىٰكَ حَدِيثُ مُوسَىٰٓ ٩ إِذْ رَءَا نَارًا فَقَالَ لِأَهْلِهِ ٱمْكُثُوٓا۟ إِنِّىٓ ءَانَسْتُ نَارًا لَّعَلِّىٓ ءَاتِيكُم مِّنْهَا بِقَبَسٍ أَوْ أَجِدُ عَلَى ٱلنَّارِ هُدًى ١٠

{9-10} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kwa namna ya kuuliza swali balagha na kukipa taadhima kisa hiki, na kukiinua hadhi yake, "Je, imekufikia hadithi ya Musa?" Katika hali yake, ambayo ndiyo chanzo cha furaha yake na chimbuko la unabii wake. Aliona moto kwa mbali, na alikuwa amepotea njia na amepigwa na baridi, na hakuwa na kitu cha kujipasha moto kwacho katika safari yake hiyo. Basi akawaambia ahali zake, "Hakika mimi nimeuona moto." Na hilo lilikuwa upande wa kulia wa mlima. "Huenda nikawaletea kijinga kutoka humo" muweze kuuota "au nikapata wongofu kwenye moto huo." Yaani, nikapata wa kuniongoza njia. Na alikuwa anatafuta nuru na mwongozo wa kihisia, lakini akapata hapo nuru isiyokuwa ya kihisia, nuru ya Ufunuo ambayo kwayo roho na nyoyo zinapata nuru, na akapata hapo uwongofu wa uhakika hadi kwenye njia iliyonyooka ifikishayo kwenye bustani za neema. Kwa hivyo akapata jambo ambalo halikuwa katika hesabu zake wala mawazo yake.