طه
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
إِنَّآ ءَامَنَّا بِرَبِّنَا لِيَغْفِرَ لَنَا خَطَـٰيَـٰنَا وَمَآ أَكْرَهْتَنَا عَلَيْهِ مِنَ ٱلسِّحْرِ ۗ وَٱللَّهُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰٓ ٧٣
{73} "Hakika sisi tumemuamini Mola wetu Mlezi ili atusamehe makosa yetu." Yaani, ukafiri wetu na maasia yetu. Kwa maana imani inafuta mabaya, nayo toba inafuta yote yaliyokuwa kabla yake. Na kauli yao, "na uchawi uliotulazimisha kuufanya" ambao tuliipinga haki kwa huo. Na huu ni ushahidi kwamba hawakuwa na hiari kuhusiana na matendo yao yaliyotangulia, na ni Firauni tu aliyewalazimisha kufanya hivyo. Na ni dhahiri - na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi - kwamba Musa alipowaaidhi - kama ilivyotangulia hapo awali katika kauli yake, "Ole wenu! Msimzulie Mwenyezi Mungu uongo, akaja wafutilia mbali kwa adhabu;" alikuwa na athari kwao na ikwaingia vikubwa. Na ndiyo maana wakagombana baada ya maneno na mawaidha haya. Kisha Firauni akawalazimisha kufanya hivyo na akawalazimisha kufanya njama waliyoifanya. Na ndiyo maana wakasema maneno yake yaliyotangulia kabla ya kuja kwao. Waliposema, "Hakika hawa wawili ni wachawi, wanataka kuwatoa katika nchi yenu." Basi wakatekeleza yale aliyowawekea yeye na kuwalazimisha kufanya. Na huenda mkwaruzo huu uliotua katika nyoyo zao kutokana na kuchukia kwao kupinga haki kwa batili, na kufanya kwao yale waliyoyafanya ili yapite tu, ndio yaliyowaathiri, na Mwenyezi Mungu akawarehemu kwa sababu yake, na aauwawezesha kuamini na kutubia. "Na Mwenyezi Mungu ndiye Mbora" kuliko yale uliyotuahidi ya malipo, cheo, na heshima, "na Mwenye kudumu zaidi" katika malipo na wema, na siyo hayo anayoyasema Firauni, "na hapo kwa yakini mtajua ni nani katika sisi aliye mkali wa kuadhibu na kuiendeleza adhabu yake." Akimaanisha kwamba yeye ndiye mwenye kuadhibu zaidi na mwenye kuiendeleza zaidi adhabu yake. Na yote aliyokuja nayo miongoni mwa visa vya Musa na Firauni, Mwenyezi Mungu hutaja ndani yake anapofikia katika kisa cha wale wachawi kwamba Firauni aliwatishia kuwakata na kuwasulubisha, lakini hataji kuwa alifanya hivyo, wala haikuwahi kuja hadithi yoyote sahihi kuhusiana na hilo. Na kuwa na uhakika kwamba hilo lililotokea au halikutokea linahitaji ushahidi. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi hilo na mengineyo. [Lakini kuwatishia kwake kufanya hivyo pamoja na kwamba ana uwezo ni ushahidi ya kwamba lilitokea, na kwamba lau kuwa halikutokea, basi Mwenyezi Mungu angelilitaja, na kwa sababu ya kukubaliana kwa wasimulizi wake juu ya hilo].