انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · طه
السورة ٢٠

طه

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٨

قَالَ هِىَ عَصَاىَ أَتَوَكَّؤُا۟ عَلَيْهَا وَأَهُشُّ بِهَا عَلَىٰ غَنَمِى وَلِىَ فِيهَا مَـَٔارِبُ أُخْرَىٰ ١٨

{18} Musa akasema, ''Hii ni fimbo yangu; ninaiegemea na ninawaangushia majani kondoo na mbuzi wangu." Alitaja faida hizi mbili ndani yake: faida kwa jamii ya wanadamu, ambayo ni kwamba yeye huegemea juu yake katika kusimama kwake na kutembea kwake, ili kutokana na hilo wanyama pia waweze kupata faida, nayo ni kwamba alikuwa akiwachunga kondoo na mbuzi. Na anapokuwa anawalisha katika miti, anaipita miti ili majani yake yadondoke ili kondoo na mbuzi wayale. Na hii ni tabia nzuri ya Musa, amani iwe juu yake, ambayo katika athari zake ni kuwatunza vizuri wanyama na kuwatendea wema. Na hilo lilionyesha kwamba Mwenyezi Mungu alimjali, akamchagua na akamfanya kuwa maalumu, mambo ambayo ni alama ya rehema yake Mwenyezi Mungu juu yake na hekima yake. "Tena inanifaa kwa matumizi mengine" yasiyokuwa haya mawili. Na miongoni mwa adabu za Musa, amani iwe juu yake, ni kwamba wakati Mwenyezi Mungu alipomuuliza kuhusu kile kilichokuwa mkononi mwake wa kulia, na swali lilikuwa linawezakuwa limekusudiwa kuuliza kuhusu hicho kitu chenyewe au faida zake. Kwa hivyo akamjibu Mwenyezi Mungu kuhusu hicho kitu chenyewe na faida zake.