البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا مُوسَى ٱلْكِتَـٰبَ وَقَفَّيْنَا مِنۢ بَعْدِهِۦ بِٱلرُّسُلِ ۖ وَءَاتَيْنَا عِيسَى ٱبْنَ مَرْيَمَ ٱلْبَيِّنَـٰتِ وَأَيَّدْنَـٰهُ بِرُوحِ ٱلْقُدُسِ ۗ أَفَكُلَّمَا جَآءَكُمْ رَسُولٌۢ بِمَا لَا تَهْوَىٰٓ أَنفُسُكُمُ ٱسْتَكْبَرْتُمْ فَفَرِيقًا كَذَّبْتُمْ وَفَرِيقًا تَقْتُلُونَ ٨٧
(87) Mwenyezi Mungu Mtukufu anasimulia hisani yake juu ya Wana wa Israili kwamba aliwatumia Musa ambaye alizungumza naye (moja kwa moja), na akampa Taurati. Kisha akafuatisha baada yake Mitume wanaohukumu kwa Taurati, mpaka alipowahitimisha Manabii wao kwa Isa [Ibn Maryam] amani iwe juu yake. Na akampa katika ishara zilizo wazi wanazoamini wanadamu mfano wake. "Na tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu." Wafasiri wengi walisema kuwa yeye ni Jibril, amani iwe juu yake, na ikasemwa kuwa ni imani ambayo Mwenyezi Mungu anawaunga nayo mkono waja wake. Kisha pamoja na hizi neema ambazo thamani yake haikadiriki walipowajia "kwa yale ambayo hayapendwi na nafsi zenu, mlijivuna" mkaacha kuwaamini, "hivyo basi, kundi" miongoni mwao "mkawakanusha, na kundi lingine mkawauwa." Basi mkatanguliza matamanio yenu juu ya uongofu, na mkaipendelea dunia juu ya Akhera. Na ndani yake kuna makemeo na kuwafanyia ukali kwa namna isiyofichika.