البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَفَتَطْمَعُونَ أَن يُؤْمِنُوا۟ لَكُمْ وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلَـٰمَ ٱللَّهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُۥ مِنۢ بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ٧٥
(75) Huku ni kukata matumaini ya Waumini katika kuamini kwa Watu wa Kitabu. Yani msitumai kuwa wataamini, hali ya kuwa maadili yao hayaambatani na kuwa na matumaini juu yao. Kwa maana, walikuwa wakiyabadili maneno ya Mwenyezi Mungu baada ya kuyafahamu na kuyajua. Wakawa wanayawekea maana ambazo Mwenyezi Mungu hakuzitaka, ili wawafanye watu kufikiria kwamba yametoka kwa Mwenyezi Mungu, na wala hayakutoka kwa Mwenyezi Mungu. Basi ikiwa hali yao katika Kitabu chao ambacho wanakiona kuwa ndiyo heshima yao na dini yao, wanachozuia kwacho watu njia ya Mwenyezi Mungu, basi inawezekanaje kutarajiwa kutoka kwao kwamba watawaamini nyinyi? Basi hiki ni katika vitu vya mbali zaidi.