انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · البقرة
السورة ٢

البقرة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٧١

قَالَ إِنَّهُۥ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ لَّا ذَلُولٌ تُثِيرُ ٱلْأَرْضَ وَلَا تَسْقِى ٱلْحَرْثَ مُسَلَّمَةٌ لَّا شِيَةَ فِيهَا ۚ قَالُوا۟ ٱلْـَٔـٰنَ جِئْتَ بِٱلْحَقِّ ۚ فَذَبَحُوهَا وَمَا كَادُوا۟ يَفْعَلُونَ ٧١

(71) "Akasema: Yeye anasema: Kuwa huyo ni ng'ombe asiyetiwa kazini" yani aliyedunishwa kwa kazi "kulima ardhi wala kumwagia maji mimea, yu salama," hana kasoro zozote au ni salama kutokana na kulima "hana baka." Yani hakuna rangi ndani yake zaidi ya rangi iliyoelezwa hapo juu "Wakasema: Sasa umeleta (jambo la) haki." Yani ubainisho wa wazi. Na hili ni kutokana na ujinga wao. Vinginevyo, bila shaka alikwishawajia na haki mara ya kwanza. Lau kuwa walimleta ng'ombe yeyote, basi kile kilichokusudiwa kingetokea. Lakini walijifanyia ugumu kwa maswali mengi. Basi Mwenyezi Mungu akawafanyia ugumu. Na lau kuwa hawawakusema, "In shaa Allah (Mwenyezi Mungu akipenda)", pia wasingeliongoka kwa hilo. "Basi wakamchinja" yani yule ng'ombe aliyeelezwa kwa sifa hizo. "Na walikaribia mno kuwa wasifanye hayo." Kwa sababu ya ukaidi uliotokea kutoka kwao.