البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَبَدَّلَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ قَوْلًا غَيْرَ ٱلَّذِى قِيلَ لَهُمْ فَأَنزَلْنَا عَلَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ رِجْزًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ بِمَا كَانُوا۟ يَفْسُقُونَ ٥٩
(59) "Lakini waliodhulumu waliibadili" miongoni mwao. Na wala hakusema "lakini walibadili." Kwa kuwa siyo wote walikuwa wamebadili "kauli isiyo kuwa waliyoambiwa." Na badala ya "Tusamehe" wakasema "punje katika ngano," huku wakipuuza amri ya Mwenyezi Mungu, na kwa kejeli. Na ikiwa waliibadilisha kauli hiyo pamoja na wepesi wake, basi kubadilisha kwao kitendo ni katika mlango wa uwezekano mkubwa na ufaao zaidi. Na kwa sababu ya hilo, wakaingia wakitambaa juu ya makalio yao. Na kulipokuwa huku kupindukia ndiyo iliyokuwa sababu kubwa ya kuwashukia adhabu ya Mwenyezi Mungu, akasema: "Kwa hivyo tukaiteremsha juu ya wale waliodhulumu adhabu kutoka mbinguni." Kwa sababu ya kupindukia kwao mipaka na kufanya kwao jeuri.