البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أُو۟لَـٰٓئِكَ عَلَىٰ هُدًى مِّن رَّبِّهِمْ ۖ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُفْلِحُونَ ٥
(5) “Hao” yani wale walioelezwa kwa sifa njema hizi “wapo juu ya uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi;” yaani, juu ya uwongofu mkubwa, kwa sababu ukawaida (yaani siyo jina maalum) uliopo ndani yake (yaani neno uwongofu) umekusudiwa kutukuza. Na uwongofu upi ambao ni mkubwa kuliko zile sifa zilizotajwa ambazo zinajumuisha itikadi (Imani) sahihi na matendo yaliyonyooka? Na je, sivyo kuwa uwongofu wa hakika siyo isipokuwa uwongofu wao, na kishichokuwa hilo katika yale yanayoupinga basi ni upotovu? Na alitumia neno "’alaa" (juu ya) mahali hapa kuashiria (hali ya) kuwa juu. Na katika upotovu hutumia neno “fii (katika).” Kama katika kauli yake, “Na hakika sisi au nyinyi bila ya shaka tuko juu ya uwongofu au katika upotovu ulio wazi;” kwa sababu mwenye uwongofu yuko juu (ametukuka) kwa sababu ya uwongofu, na yuko juu na ameinuka kwa sababu yake; naye mwenye upotovu amedidimia ndani yake, na anadharauliwa. Kisha akasema “na hao ndio waliofaulu;” na kufaulu ni kufikia mahitaji na kuokoka kutokana na chenye kuhofisha. Na amethibiti kufaulu katika hao peke yao kwa sababu hakuna njia ya kufaulu isipokuwa kwa kufuata njia yao. Na zisizokuwa njia hiyo ni njia za upotovu, maangamio na hasara ambazo humpeleka mwenye kuzifuata katika maangamio. Kwa sababu hiyo, alipotaja sifa za Waumini wa kweli, alitaja sifa za makafiri wanaodhihirisha ukafiri wao, wanaompinga Mtume, akasema: