البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَٱسْتَعِينُوا۟ بِٱلصَّبْرِ وَٱلصَّلَوٰةِ ۚ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى ٱلْخَـٰشِعِينَ ٤٥
(45) Mwenyezi Mungu aliwaamrisha kutafuta msaada katika mambo yao yote kwa subira ya kila aina, nayo ni kusubiri juu ya kumtii Mwenyezi Mungu mpaka alifanye (jambo hilo). Na kusubiri juu ya kumuasi Mwenyezi Mungu mpaka aliache (jambo hilo). Na kusubiri juu ya makadirio machungu ya Mwenyezi Mungu; na asiyachukie. Hivyo basi, kwa subira na kujizuia nafsi juu ya yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu kusubiri juu yake ni msaada mkubwa katika kila jambo miongoni mwa mambo. Na mwenye kujisubirisha, basi Mwenyezi Mungu atampa subira. Kadhalika swala ambayo ni mizani ya imani, na inakataza mtu machafu na maovu, inatafutwa kwayo msaada juu ya kila jambo miongoni mwa mambo. "Na kwa hakika, jambo hilo," yani swala, "ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu" kwani ni rahisi na hafifu kwao. Kwa sababu, kumnyenyekea Mwenyezi Mungu, na kutaraji yaliyoko kwake, yanamletea kuifanya kwa kifua kikunjufu akitafuta (kutaraji) malipo mazuri na akihofu adhabu. Tofauti na asiyekuwa hivyo. Yeye hana haja inayomwita kuiendea. Na anapoifanya, inakuwa katika mambo mazito zaidi kwake. Na khushuu' ni kunyenyekea kwa moyo na kutua kwake, na kutulia kwake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kuvunjika kwake mbele yake kwa unyonge na kuonyesha haja kubwa, na kumwamini, na kukutana naye. Ndio maana akasema: