البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَا تَلْبِسُوا۟ ٱلْحَقَّ بِٱلْبَـٰطِلِ وَتَكْتُمُوا۟ ٱلْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ٤٢
(42) "Wala msichanganye kweli na uongo na mkaificha kweli," basi akawakataza mambo mawili: Kuchanganya haki (kweli) na batili (uwongo), na kuificha haki. Kwa sababu, kilichokusudiwa na "watu wa vitabu na elimu” ni kupambanua haki [kutoka kwa batili], na kudhihirisha haki, ili waongofu waongoke kwa hilo, na warejee waliopotea; na hoja isimame juu ya wakaidi. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu alizipambanua ishara (aya) zake na akazibainisha hoja zake zilizo wazi; ili haki ipambanuke kutoka kwa batili, na ili ibainike njia ya walioongoka kutokana na njia ya wakosefu. Basi mwenye kufanya hivi katika watu wa elimu; basi yeye ni katika washikilizi wa Mitume na viongozi wa umma. Na mwenye kuchanganya haki na batili, na hakutofautisha hili kutoka kwa lile pamoja na kujua kwake hilo, na akaficha haki anayoijua, na akaamrishwa kuidhihirisha, basi yeye ni miongoni mwa walinganiaji wa Jahannam (motoni); kwa sababu, watu katika mambo ya dini yao, hawafuati wasiokuwa wanachuoni wao. Basi zichagulieni nafsi zenu moja ya hizo hali mbili.