البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَقُلْنَا يَـٰٓـَٔادَمُ ٱسْكُنْ أَنتَ وَزَوْجُكَ ٱلْجَنَّةَ وَكُلَا مِنْهَا رَغَدًا حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَـٰذِهِ ٱلشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ ٣٥
(35) Mwenyezi Mungu alipomuumba Adam na akamfanya kuwa bora, akakamilisha neema zake juu yake; kwamba alimuumba kutokana naye mke; ili akae naye kwa utulivu na usuhuba. Akawaamrisha waishi Peponi, na wale humo raghadan (yani kwa upana maridhawa) “popote mpendapo” yani katika aina mbalimbali za thimaar (mazao) na matunda. Na Mwenyezi Mungu akamwambia: “Hakika humo hutakuwa na njaa wala hutakuwa uchi. Na hakika, hutapata kiu humo wala hutapata joto.” “Lakini msiukaribie mti huu tu;” aina moja katika aina za miti ya Peponi. Mwenyezi Mungu ndiye anayeujua zaidi. Lakini aliwakataza mti huo ili kuwapa mtihani na majaribio au kwa sababu ya hekima tusiyoijua. “Mkawa katika wale waliodhulumu.” Inaonyesha kwamba huko kukataza kulikuwa kwa kuharamisha, kwa sababu alikufungamanisha na dhuluma. Basi adui yao hakuacha kuwashawishi, na kuwapambia kula kile walichokatazwa, mpaka akawatelezesha kwa kuwapambia. “Naye akawaapia” kwa jina la Mwenyezi Mungu. “Kwa yakini, mimi ni miongoni mwa wanaokusihini.”