البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَىٰهُمْ وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ يَهْدِى مَن يَشَآءُ ۗ وَمَا تُنفِقُوا۟ مِنْ خَيْرٍ فَلِأَنفُسِكُمْ ۚ وَمَا تُنفِقُونَ إِلَّا ٱبْتِغَآءَ وَجْهِ ٱللَّهِ ۚ وَمَا تُنفِقُوا۟ مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ ٢٧٢
{272} Yani, ewe Mtume kilicho juu yako ni kufikisha tu na kuwahimiza watu kutenda mema, na kuwakemea kutokana na maovu. Ama uwongofu, basi hilo limo mkononi mwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na anajulisha kuhusu Waumini wa kweli kwamba wao hawatoi ispokuwa kwa kutaka radhi ya Mola wao Mlezi, na kutarajia thawabu yake. Kwa sababu imani yao inawaita katika hayo. Na hili ndio utakaso bora wa Waumini. Na inajumuisha kuwakumbusha kuwa na ikhlasi. Na alirudia elimu yake yeye Mtukufu kuhusu kutoa kwa matumizi ili kuwajulisha kuwa Yeye haupotei kwake uzito wa chembe. Hata kama ni wema mmoja, yeye huuzidisha, na hupeana kutoka kwake malipo makubwa.