البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
مَّثَلُ ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَٰلَهُمْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنۢبَتَتْ سَبْعَ سَنَابِلَ فِى كُلِّ سُنۢبُلَةٍ مِّا۟ئَةُ حَبَّةٍ ۗ وَٱللَّهُ يُضَـٰعِفُ لِمَن يَشَآءُ ۗ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٌ ٢٦١
{261} Huku ni kuhimiza kukubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake juu ya kutoa mali zao katika njia yake. Nayo ni njia yake inayofikisha kwake. Kwa hivyo, inaingia katika hili kutoa kwake kwa ajili ya kukuza elimu zenye manufaa. Na katika kutayarisha jihadi katika njia yake, na katika kujitayarisha na kuwaandaa wale wanaopigana katika Jihadi, na katika miradi yote ya heri yenye manufaa kwa Waislamu. Kisha hilo linafuatwa na kuwapa wenye mahitaji, na mafakiri, na masikini. Na inawezekana mambo mawili haya kukutana, basi ikawa katika kutoa kuna kuondoa mahitaji na kusaidia katika heri na utiifu. Kwa hivyo, kutoa huku kwa ajili ya matumizi kunazidishwa kuzidisha huku mara mia saba hadi zaidi ya hapo. Na ndio maana akasema, “na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye.” Na hilo ni kulingana na yale yaliyomo katika moyo wa mtoaji ya imani na ikhlasi kamili, na katika matunda ya aliyotoa kwa ajili ya matumizi na manufaa yake. Kwa maana, baadhi ya njia za heri, matokeo ya kutoa matumizi katika hizo huwa yenye manufaa ya kuendelea, na masilahi mbalimbali. Basi yakawa malipo ni ya aina sawa na matendo.