انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · البقرة
السورة ٢

البقرة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٥٧

ٱللَّهُ وَلِىُّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ يُخْرِجُهُم مِّنَ ٱلظُّلُمَـٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ ۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ أَوْلِيَآؤُهُمُ ٱلطَّـٰغُوتُ يُخْرِجُونَهُم مِّنَ ٱلنُّورِ إِلَى ٱلظُّلُمَـٰتِ ۗ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلنَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ ٢٥٧

{257} Aya hii inafuata Aya iliyotangulia, kwa hivyo iliyo tangulizi ndiyo msingi, na hii ndiyo matunda. Basi Mola Mtukufu akajulisha kwamba wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na wakasadikisha imani yao kwa kutekeleza wajibu wa imani na kuacha kila kinachopingana nayo. Kwamba Yeye ndiye Mlinzi wao anayewasimamia kusimamia kwake maalumu, na anayasimamia malezi yao. Kwa hivyo, huwatoa katika giza mbalimbali la ujinga na ukafiri na maasia na kughafilika na kupeana mgongo hadi katika nuru ya elimu, na yakini, na imani, na utiifu, na kumwelekea Mola wa Mlezi kikamilifu. Na anaziangaza nyoyo zao kwa yale anayoyatia ndani yake ya nuru ya Wahyi na imani. Na anawasahilishia yawe mepesi, na anawaepushia ugumu. Na ama wale waliokufuru, wao walipomfanya asiyekuwa mlinzi wao kuwa rafiki yao, Mwenyezi Mungu aliwaachia wale walichojifanyia wenyewe kuwa rafiki yao. Na akaacha kuwasaidia, na akawakabidhi katika uangalizi wa wale waliowafanya kuwa rafiki miongoni mwa wale wasiofaidi wala kudhuru. Wakawafanya kuwa wapotovu, na wakawanyima uongofu wa elimu yenye manufaa na matendo mema, na wakawanyima furaha, na Moto ukawa ndio makazi yao, watakaa humo milele. Ewe Mwenyezi Mungu, kuwa mlinzi wetu katika wale unaowalinda.