البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَإِنْ عَزَمُوا۟ ٱلطَّلَـٰقَ فَإِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ٢٢٧
{227} “Na wakiazimia kuwapa talaka.” Yani wakikataa kuwarudia wake zao, hilo litakuwa dalili ya kutowapenda kwao na kutowataka wake zao. Na hili haliwi isipokuwa ni kuazimia kufanya talaka. Na hili likifanyika, basi atalazimika kumpa talaka mara moja, vinginevyo mtawala atamlazimisha kuifanya au yeye mwenyewe atafanya hivyo. “Basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.” Ndani yake kuna onyo na tishio kwa mwenye kuapa kiapo hiki, na akakusudia kwacho kudhuru na kufanya ugumu. Na Aya hii inatumika kama dalili kwamba Al-iilaa ni mahususi tu kwa mke, kwa sababu ya kauli yake, “wake zao.” Na pia juu ya kwamba ni wajibu kujamiiana mara moja kila baada ya miezi minne. Kwa sababu, baada ya miezi minne, atalazimishwa ima kufanya jimai au talaka. Na hilo haliwi isipokuwa kwa sababu ameacha la wajibu.