البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱدْخُلُوا۟ فِى ٱلسِّلْمِ كَآفَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا۟ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيْطَـٰنِ ۚ إِنَّهُۥ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ٢٠٨
{208} Hii ni amri kutoka kwa Mola Mtukufu kwa Waumini kwamba waingie, “Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu.” Yani katika sheria zote za dini, wala wasiache chochote chake, na kwamba wasiwe miongoni mwa wale walioyafanya matamanio yao kuwa ndiyo mungu wao. Ikiwa jambo lililo katika sheria litakubaliana na matamanio yao, analifanya. Na likitofautiana nayo, analiacha. Lakini, wajibu ni kwamba matamanio yafuate dini, na kwamba yote anayoweza katika matendo mema. Na yale asiyoyaweza, anayawekea azma, na anayatilia nia, kwa hayo anayapata kwa nia yake. Na kwa kuwa kuingia katika Uislamu kwa ukimilifu hakuwezekani kuingia akilini isipokuwa kwa kuhalifu njia za Shetani, akasema; “wala msifuate nyayo za Shetani.” Yani katika kumuasi Mwenyezi Mungu. “Hakika, yeye kwenu ni adui wa dhahiri.” Na adui wa dhahiri haamrishi isipokuwa uovu na machafu, na yale yenye kuwadhuru. Na kwa kuwa mja hana budi kufanya kosa na kuteleza, Mola Mtukufu akasema: