انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · البقرة
السورة ٢

البقرة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٠٤

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُعْجِبُكَ قَوْلُهُۥ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَيُشْهِدُ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا فِى قَلْبِهِۦ وَهُوَ أَلَدُّ ٱلْخِصَامِ ٢٠٤

Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoamrisha kumtaja kwa wingi hasa katika nyakati bora, ambalo (yani kumtaja) ni heri na lenye masilahi na wema. Yeye Mtukufu akajulisha kuhusu hali ya yule anayezungumza kwa ulimi wake na kitendo chake kinapingana na kauli yake. Na mazungumzo ima humnyanyua mtu au humshusha. Akasema: “Na katika watu yupo yule ambaye maneno yake kwa maisha ya kidunia hukupendeza.” Yani anapozungumza, maneno yake yanamvutia msikilizaji. Na anapotamka utamdhania anazungumza maneno yenye manufaa, na anayasisitiza anayoyasema kuwa: “Humshuhudisha Mwenyezi Mungu kwa yaliyomo katika moyo wake;” kwa kusema kuwa Mwenyezi Mungu anajua kwamba yale yaliyomo ndani ya moyo wake yanaafikiana na yale aliyotamka. Ilhali yeye ni mwongo katika hayo, kwa sababu kauli yake inapingana na kitendo chake. Na lau kuwa alikuwa mkweli, maneno yake na vitendo vyake vingeafikiana, kama ilivyo hali ya Muumini asiyekuwa mnafiki. Ndio maana akasema, “na hali yeye ndiye mgomvi mkubwa mno.” Yani unapogombana naye, utakuta ndani yake ugomvi mkubwa, na ugumu na kutetea batili. Na yale yanayotokana na hayo ambayo ni katika sifa mbaya. Si kama tabia za Waumini ambao walifanya wepesi ndiyo kipando chao, na kufuata haki ndiyo kazi yao, na uzuri katika kuamiliana ndiyo tabia yao.