البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ثُمَّ أَفِيضُوا۟ مِنْ حَيْثُ أَفَاضَ ٱلنَّاسُ وَٱسْتَغْفِرُوا۟ ٱللَّهَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ١٩٩
“Kisha miminikeni kutoka pale wanapomiminika watu,” yani kisha miminikeni kutoka Muzdalifah kutoka pale ambapo watu wanamiminika tangu siku za Ibrahim, amani iwe juu yake, mpaka sasa. Na kilichokusudiwa na kuunganisha huku (yani kutoka pale wanapomiminika watu) kilikuwa kinajulikana kwao (yani Maqureshi). Ambayo ni kutupa vijiwe kwenye Al-Jamarat, kuchinja dhabihu, kuzunguka Al-Ka’aba, kufanya Sa’ayi, kulala Mina katika siku za At-Tashriq na kukamilisha ibada zinginezo za Hijja. Na kwa vile [huku] kumiminika kusudi lake ni hayo yaliyotajwa, na kwamba yaliyotajwa ndiyo mambo ya mwisho wa ibada za Hijja. Yeye Aliyetukuka aliamrisha baada ya kuikamilisha kumwomba msamaha na kumtaja kwa wingi. Na kuomba msamaha ni kwa sababu ya makosa yaliyotokea kutoka kwa mja katika kutekeleza ibada zake na mapungufu yake ndani yake. Na kumtaja Mwenyezi Mungu ni kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema yake juu yake kwa kumwezesha kufanya hii ibada tukufu na neema kubwa mno. Hivyo basi, mja anafaa kila anapomaliza ibada, amuombe msamaha Mwenyezi Mungu kwa upungufu wake. Na amshukuru kwa kumwezesha, na siyo kama yule anayeona kwamba amekamilisha ibada. Hivyo akaona kuwa amemfanyia hisani Mola wake Mlezi kwa kuifanya na kwamba itampa cheo na hadhi ya juu. Basi huyu anastahiki kuchukiwa na kukataliwa matendo yake, kama vile yule wa kwanza anavyostahiki kukubaliwa matendo na kuwezeshwa kufanya matendo mengine.