البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَقَـٰتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ ٱلدِّينُ لِلَّهِ ۖ فَإِنِ ٱنتَهَوْا۟ فَلَا عُدْوَٰنَ إِلَّا عَلَى ٱلظَّـٰلِمِينَ ١٩٣
Kisha Yeye Mtukufu akataja lengo la kupigana katika njia yake. Na kwamba haikusudii kumwaga damu za makafiri na kuchukua mali zao. Bali kinachokusudiwa kwayo ni kuwa, “Dini iwe tu ya Mwenyezi Mungu” Mtukufu. Ili Dini ya Mwenyezi Mungu [Mtukufu] idhihiri dini nyingine zote, na kizuiwe kila kinachoipinga, kama vile ushirikina na mengineyo, ambayo ndiyo iliyokusudiwa na fitina. Na makusudio haya yanapopatikana, basi hakuna kuua wala kupigana, “wakiacha” kuwapiga katika Msikiti Mtakatifu. “Basi usiwepo uadui isipokuwa kwa madhulumu,” yani wasishambulie na yeyote katika nyinyi, isipokuwa mwenye kudhulumu miongoni mwao. Basi huyo anastahili kuadhibiwa, kwa kiwango cha dhuluma yake.