انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · البقرة
السورة ٢

البقرة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ١٧٤–١٧٥

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلْكِتَـٰبِ وَيَشْتَرُونَ بِهِۦ ثَمَنًا قَلِيلًا ۙ أُو۟لَـٰٓئِكَ مَا يَأْكُلُونَ فِى بُطُونِهِمْ إِلَّا ٱلنَّارَ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ ٱللَّهُ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ١٧٤ أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ٱشْتَرَوُا۟ ٱلضَّلَـٰلَةَ بِٱلْهُدَىٰ وَٱلْعَذَابَ بِٱلْمَغْفِرَةِ ۚ فَمَآ أَصْبَرَهُمْ عَلَى ٱلنَّارِ ١٧٥

(174 - 175) Hili ni tishio kali kwa wale wanaoficha yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwa Mitume wake katika elimu, ambayo Mwenyezi Mungu alichukua agano juu ya watu wake. Kwamba waibainishe kwa watu na wala wasiifiche. Basi mwenye kuibadilisha kwa takataka za kidunia, na akaficha amri ya Mwenyezi Mungu, basi hao “hawali katika tumbo zao isipokuwa moto.” Kwa sababu hiyo ndiyo thamani waliyoichuma, lakini iliwafikia kwa mapato mabaya mno, haramu iliyo kubwa zaidi. Kwa hivyo malipo yao yakawa ya aina sawa na matendo yao, “wala Mwenyezi Mungu hatawaongelesha Siku ya Kiyama.” Bali alikwisha wakasirikia na akawapa mgongo. “Wala hatawatakasa,” yani hatawatakasa kutokana na tabia chafu. Na wala hawana matendo yanayostahiki sifa, kuridhiwa, na malipo juu yake. Na hakuwatakasa kwa sababu, walifanya sababu za kutowatakasa ambako (huko kutakaswa) sababu zake kubwa ni kufanya matendo kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na kuongoka kukielekea, na kukilingania. Lakini hawa walikitupa Kitabu cha Mwenyezi Mungu, wakakipa mgongo, na wakachagua upotovu badala ya uwongofu, na adhabu badala ya msamaha. Kwa hivyo hawa (watu) hakiwafai kitu isipokuwa moto, basi vipi watakuwa na subira juu yake (moto), na ni vipi watakuwa na stahmala juu yake?