البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ كُلُوا۟ مِن طَيِّبَـٰتِ مَا رَزَقْنَـٰكُمْ وَٱشْكُرُوا۟ لِلَّهِ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ ١٧٢
Hii ni amri kwa Waumini hasa, baada ya amri ya jumla. Na hilo ni kwa sababu wao ndio wanaonufaika kwa hakika na maamrisho na makatazo, kwa sababu ya imani yao. Kwa hivyo, akawaamrisha kula vitu vizuri katika riziki, na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema zake, kwa kuzitumia katika kumtii; na kupata nguvu kwavyo kwa yale yanayofikisha kwake. Hivyo, akawaamrisha yale aliyowaamrisha Mitume katika kauli yake. “Enyi Mitume, kuleni katika vizuri na tendeni mema.” Basi kushukuru katika Aya hii ni matendo mema. Na hapa hakusema “halali” kwa sababu, Mwenyezi Mungu alimruhusu Muumini kula vitu vizuri kutoka katika riziki ilimradi visiwe na matokeo yoyote mabaya. Na kwa sababu imani yake inamzuia kula kisichokuwa chake. Na kauli yake “ikiwa kweli mnamuabudu Yeye tu,” yani mshukuruni. Kwa hivyo, inaashiria kwamba yule asiyemshukuru Mwenyezi Mungu, basi hajamuabudu Yeye peke yake. Kama vile mwenye kumshukuru atakuwa amemuabudu, na amefanya yale aliyoamrishwa. Na pia inaashiria kwamba kula vilivyo vizuri ni sababu ya kutenda mema na kukubaliwa kwake. Na amri ya kushukuru baada ya kuneemeshwa ni kwa sababu shukrani huhifadhi neema zilizopo, na huleta neema zisizokuwepo. Kama vile kufuru hufukuza neema zisizokuwepo na huondoa neema zilizopo.