انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · البقرة
السورة ٢

البقرة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٥

ٱللَّهُ يَسْتَهْزِئُ بِهِمْ وَيَمُدُّهُمْ فِى طُغْيَـٰنِهِمْ يَعْمَهُونَ ١٥

(15) Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Mwenyezi Mungu atawadhihaki wao na atawaacha katika upotovu wao wakitangatanga ovyo." Na haya ni malipo yao kwa kukejeli kwao waja wake. Na katika kejeli yake (Mwenyezi Mungu) kwao ni kwamba aliwapambia maovu ambayo wamo ndani yake na hali zao mbaya, mpaka wakadhani kuwa wako pamoja na Waumini pindi Mwenyezi Mungu alipoacha kuwapa Waumini mamlaka juu yao. Na katika kejeli yake kwao Siku ya Kiyama ni kwamba atawapa nuru iliyo dhahiri pamoja na Waumini. Na Waumini watakapokwenda na nuru yao, nuru ya wanafiki itazimika, na watabaki wamechanganyikiwa gizani baada ya kuwa na nuru. Basi ni kukata tamaa kulikoje huku baada ya kuwa na matumaini. "Watawaita (wawaambie): Kwani hatukuwa pamoja nanyi? Watawaambia: Ndiyo, lakini mlijifitini wenyewe, na mkangoja, na mkatia shaka..." hadi mwisho wa aya. Kauli yake "na atawaacha;" yaani, atawazidishia muhula "katika upotovu wao" yani uovu wao na ukafiri wao; "wakitangatanga ovyo" yaani, huku wamechanganyikiwa na kusitasita. Na hii ni katika kejeli yake (Mwenyezi Mungu) Mtukufu kwao.