انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · البقرة
السورة ٢

البقرة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٤٦

ٱلَّذِينَ ءَاتَيْنَـٰهُمُ ٱلْكِتَـٰبَ يَعْرِفُونَهُۥ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَآءَهُمْ ۖ وَإِنَّ فَرِيقًا مِّنْهُمْ لَيَكْتُمُونَ ٱلْحَقَّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ١٤٦

(146) Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha ya kwamba Watu wa Kitabu imekwisha thibiti kwao na wakajua ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kwamba aliyokuja nayo ni haki na ukweli. Na wakawa na yakini na hilo kama walivyo na yakini juu ya watoto wao kwa namna kwamba, hawawafananii kama watoto wengine. Basi elimu yao juu ya Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - ilifikia kiwango ambacho hawana shaka ndani yake, wala hawana wasiwasi wowote. Lakini, kundi miongoni mwao, nao ndio wengi wao, ambao walimkufuru, waliuficha ushuhuda huu pamoja na kuwa na yakini juu yake hali ya kuwa wanajua. Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayeficha ushahidi alionao kutoka kwa Mwenyezi Mungu? Na ndani ya hayo, kuna kumfariji Mtume na Waumini, na ni kuwatahadharisha kutokana na maovu yao na fikira zao potofu. Na kundi miongoni mwao halikuificha haki hali ya kuwa wanajua. Basi, wapo miongoni mwao walioiamini, na miongoni mwao wapo walioikufuru kwa kutojua. Hivyo basi, mwanachuoni hana budi kuidhihirisha haki, kuibainisha, na kuipamba kwa kila neno awezalo, dalili, mfano, na yasiyokuwa hayo. Na kuibatilisha batili (uwongo), kuipambanua kutokana na haki, kuidhalilisha, na kuifanya kuwa mbaya katika nafsi kwa kila njia ifikishayo kwa hilo. Basi, hawa wafichaji waligeuza jambo hili, basi hali zao zikawa kinyume.