البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَمْ كُنتُمْ شُهَدَآءَ إِذْ حَضَرَ يَعْقُوبَ ٱلْمَوْتُ إِذْ قَالَ لِبَنِيهِ مَا تَعْبُدُونَ مِنۢ بَعْدِى قَالُوا۟ نَعْبُدُ إِلَـٰهَكَ وَإِلَـٰهَ ءَابَآئِكَ إِبْرَٰهِـۧمَ وَإِسْمَـٰعِيلَ وَإِسْحَـٰقَ إِلَـٰهًا وَٰحِدًا وَنَحْنُ لَهُۥ مُسْلِمُونَ ١٣٣
(133) Na Mayahudi walipokuwa wakidai kuwa wao wako katika mila ya Ibrahim na baada yake Yaaqub, Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema huku akiwakanusha. "Je! Mlikuwapo" yani mlihudhuria "yalipomfikia Yaaqub mauti" yani vitangulizi vyake, na sababu zake. Hivyo, akawaambia wanawe katika hali ya kuwapa mtihani, na ili lifurahie jicho lake katika uhai wake kwa kufuata kwao yale aliyowausia. "Mtamuabudu nani baada yangu?" Basi wakamjibu kwa yale yaliofurahisha jicho lake, wakasema "Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is-hak, Mungu Mmoja tu." Na wala hatumshirikishi na chochote, wala hatumsawazishi na chochote "na sisi tunasilimu kwake". Basi wakajumuisha baina ya Tauhid na vitendo. Na linalojulikana ni kwamba wao hawakumhudhuria Yaaqub, kwa sababu hawakuwa wemeumbwa bado. Na ikiwa hawakuhudhuria, basi Mwenyezi Mungu alikwisha waambia kuwa aliwausia watoto wake kwa Hanifiyya (kuelekea kwa Mwenyezi Mungu peke yake na kujiepusha na vinginevyo), na sio kwa Uyahudi. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: