البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ ءَامِنُوا۟ كَمَآ ءَامَنَ ٱلنَّاسُ قَالُوٓا۟ أَنُؤْمِنُ كَمَآ ءَامَنَ ٱلسُّفَهَآءُ ۗ أَلَآ إِنَّهُمْ هُمُ ٱلسُّفَهَآءُ وَلَـٰكِن لَّا يَعْلَمُونَ ١٣
(13) Yaani wanapoambiwa wanafiki “Aminini kama walivyoamini watu,” yaani, kama imani ya maswahaba radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, ambayo ni imani kwa moyo na ulimi. Wanasema kwa madai yao ya uwongo, "tuamini kama walivyoamini wapumbavu?" Wakimaanisha - Mwenyezi Mungu awalaani - maswahaba, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao; wakidai kwamba upumbavu wao (maswahaba) uliwafanya kuamini, na kuondoka katika nchi zao, na kuwafanyia uadui makafiri. Lakini akili zao (wanafiki) zikaona kwamba kinyume cha hayo ndicho kilifaa, hivyo basi wakawanasibisha (maswahaba) na upumbavu. Na ndani ya hilo ni kwamba wao ndio wenye hekima zaidi, wababe wa ufahamu na akili. Lakini Mwenyezi Mungu akawajibu hilo, na akasema kwamba wao ndio wapumbavu kwa hakika. Kwa sababu uhakika wa upumbavu ni mtu kutojua masilahi ya nafsi yake, na akawania katika yale yenye kuidhuru, na sifa hii inawafaa zaidi, [na ni ya ukweli juu yao]. Kama vile akili na ujuzi ni mtu kujua masilahi ya nafsi yake na akawania katika yale yenye kumnufaisha, na katika kuzuia yale yenye kumdhuru. Na sifa hii inawafaa maswahaba na Waumini. Kwa hivyo, la kuzingatiwa ni sifa (maelezo) na dalili, siyo madai tu na maneno matupu.