البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
رَبَّنَا وَٱجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَآ أُمَّةً مُّسْلِمَةً لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَآ ۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ ١٢٨
(128) Na walijiombea nafsi zao na vizazi vyao kwamba wawe Waislamu. Ambao uhakika wake ni kunyenyekea moyo na kufuata kwake Mola wake Mlezi, ambako kunajumuisha kufuata kwa viungo. "Na utuonyeshe njia za ibada yetu," yani tufundishe hayo kwa njia ya kuonyesha na kushuhudia, ili iwe yenye kuathiri zaidi. Na inawezekana kwamba kinachokusudiwa na manasik ni matendo yote ya Hijja, kama inavyoashiriwa na muktadha na mahali. Na inawezekana kwamba kinachokusudiwa ni cha jumla zaidi ya hilo, nacho ni dini yote na ibada zote mbalimbali; kama inavyoashiriwa na ujumla wa neno hili. Kwa sababu, nusuk ni kuabudu, lakini limetumika sana kidesturi katika ibada mbalimbali za Hijja. Kwa hivyo, yanakuwa matokeo ya dua yao ni yenye kurudi kwa kuwezeshwa kuwa na elimu yenye manufaa na matendo mema. Na kwa vile mja, hata aweje, ni lazima apatwe na mapungufu na ahitaji kutubia, akasema, "na utusamehe. Bila shaka, Wewe ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu."