البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَإِذْ قَالَ إِبْرَٰهِـۧمُ رَبِّ ٱجْعَلْ هَـٰذَا بَلَدًا ءَامِنًا وَٱرْزُقْ أَهْلَهُۥ مِنَ ٱلثَّمَرَٰتِ مَنْ ءَامَنَ مِنْهُم بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ ۖ قَالَ وَمَن كَفَرَ فَأُمَتِّعُهُۥ قَلِيلًا ثُمَّ أَضْطَرُّهُۥٓ إِلَىٰ عَذَابِ ٱلنَّارِ ۖ وَبِئْسَ ٱلْمَصِيرُ ١٢٦
(126) Yani Ibrahim alipoiombea Nyumba hii kwamba Mwenyezi Mungu aifanye kuwa nchi yenye amani, na awaruzuku watu wake kutokana na aina za matunda. Kisha yeye, amani iwe juu yake, aliwekea hii dua kwa Waumini peke yao kwa sababu ya kuwa na adabu kwa Mwenyezi Mungu, kwa kuwa dua yake ya kwanza ilikuwa ya jumla kabisa. Basi jawabu likaja huku limewabania nje wenye kudhulumu. Kwa hivyo, alipowaombea riziki na akawikewa kwa ajili ya Muumini peke yake, na ikawa riziki ya Mwenyezi Mungu inamfikia Muumini, kafiri, muasi, na mtiifu, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na mwenye kukufuru pia" yani nitawaruzuku wote, Muislamu wao na kafiri wao. Ama Muislamu, yeye atatumia hiyo riziki katika kumwabudu Mwenyezi Mungu, kisha atatoka humo kwenda kwenye neema ya Peponi. Na ama kafiri, yeye atastarehe humo kidogo "kisha nitamsukumiza," yani nitamtoa kwa lazima na kwa nguvu kwenda "kwenye adhabu ya Moto, napo ni pahali pabaya mno pa kurejea."