البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَن تَرْضَىٰ عَنكَ ٱلْيَهُودُ وَلَا ٱلنَّصَـٰرَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى ٱللَّهِ هُوَ ٱلْهُدَىٰ ۗ وَلَئِنِ ٱتَّبَعْتَ أَهْوَآءَهُم بَعْدَ ٱلَّذِى جَآءَكَ مِنَ ٱلْعِلْمِ ۙ مَا لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن وَلِىٍّ وَلَا نَصِيرٍ ١٢٠
(120) Mwenyezi Mungu anamfahamisha Mtume wake kwamba Mayahudi wala Manaswara hawawi radhi naye isipokuwa kwa kufuata yeye dini yao. Kwa sababu, wao ni walinganizi kwa dini waliyo nayo, wakidai kuwa ndiyo uwongofu. Basi waambie "Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu" ambao nimetumwa nao "ndio uwongofu." Na ama yale mliyo nayo, hayo ni matamanio tu, kwa dalili ya kauli yake: "Na kama ukifuata matamanio yao baada ya yale yaliyokujia katika elimu, hutapata mlinzi wala msaidizi kando na Mwenyezi Mungu." Na hili lina katazo kubwa la kufuata matamanio ya Mayahudi na Wakristo, na kuwaiga katika yale ambayo ni mahususi kwa dini yao. Na ijapokuwa kauli (hii) ni ya Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani ziwe juu yake, - umma wake unaingia katika hayo. Kwa sababu, mazingatio ni katika ujumla wa maana, na sio katika umaalumu wa anayeambiwa. Kama vile mazingatio ni katika ujumla wa tamko, na sio katika umahususi wa sababu.