البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَقَالُوا۟ لَن يَدْخُلَ ٱلْجَنَّةَ إِلَّا مَن كَانَ هُودًا أَوْ نَصَـٰرَىٰ ۗ تِلْكَ أَمَانِيُّهُمْ ۗ قُلْ هَاتُوا۟ بُرْهَـٰنَكُمْ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ ١١١
(111) Yani Mayahudi walisema: Hataingia Peponi ila aliyekuwa Myahudi. Nao Wakristo wakasema: Hataingia Peponi ila aliyekuwa Mkristo. Basi wakajihukumia kwamba wao peke yao ndio watakaoingia Peponi. Na haya ni matamanio tu ambayo hayakubaliwi isipokuwa kwa hoja na dalili. Basi ileteni (hoja) ikiwa nyinyi ni wakweli. Na vivyo hivyo, kila mwenye kudai madai, ni lazima ayaletee ushahidi (dalili) juu ya usahihi wa madai yake. Vinginevyo, ikiwa madai yake yatageuzwa dhidi yake, na mwenye kudai mwingine akadai kinyume cha alichodai bila ushahidi, itakuwa hakuna tofauti yoyote kati yao. Kwa hivyo, ushahidi ndio unaosadikisha madai au uyakadhibishe. Na kwa vile hakukuwa na ushahidi mikononi mwao, ulijulikana uongo wao kwa (kudai) madai hayo.