البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَدَّ كَثِيرٌ مِّنْ أَهْلِ ٱلْكِتَـٰبِ لَوْ يَرُدُّونَكُم مِّنۢ بَعْدِ إِيمَـٰنِكُمْ كُفَّارًا حَسَدًا مِّنْ عِندِ أَنفُسِهِم مِّنۢ بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ ٱلْحَقُّ ۖ فَٱعْفُوا۟ وَٱصْفَحُوا۟ حَتَّىٰ يَأْتِىَ ٱللَّهُ بِأَمْرِهِۦٓ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ ١٠٩
(109) Kisha akajulisha kuhusu husuda ya wengi katika Watu wa Kitabu, na ya kwamba wamefikia hali ya kuwa wanatamani, "lau wangekurudisheni nyinyi muwe makafiri baada ya kuamini kwenu." Na wakafanya juhudi katika hilo, na wakafanya hila mbalimbali, lakini hila zao zinawarudia kama alivyosema Mtukufu. "Na kikundi katika Watu wa Kitabu walisema: Yaaminini yale waliyoteremshiwa wenye kuamini mwanzo wa mchana, na yakataeni mwisho wake; huenda wakarejea." Na hii ni kutokana na husuda yao itokayo katika nafsi zao. Lakini Mwenyezi Mungu akawaamrisha wakabiliane na wale waliowaudhi [vibaya mno] kwa kuwasamehe na kuwatupilia mbali mpaka Mwenyezi Mungu atakapoleta amri yake. Kisha baada ya hayo, Mwenyezi Mungu akawaletea amri yake kwamba wafanye jihadi. Hivyo basi, Mwenyezi Mungu akaziponya nafsi za Waumini kutokana nao, na wakawauwa waliowauwa, na wakawafanya watumwa, na wakawatoa wale waliowatoa. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu."