مريم
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ سَيَجْعَلُ لَهُمُ ٱلرَّحْمَـٰنُ وُدًّا ٩٦
{96} Hii ni miongoni mwa neema zake juu ya waja wake ambao waliunganisha kati ya imani na matendo mema, nayo ni kuwa aliwaahidi kwamba atawapa mapenzi katika nyoyo za vipenzi wake na wakazi wa mbinguni na ardhini. Na ikiwa wana mapenzi katika nyoyo hizo, mengi ya mambo yao yatawawia mepesi, na watapata heri nyingi, dua mbalimbali, mwongozo, kukubaliwa, na uongozi. Na ndiyo maana ikaja katika Hadithi sahihi kuwa: "Hakika Mwenyezi Mungu anapompenda mja, anamnadi Jibril: Hakika Mimi ninampenda fulani, kwa hivyo mpende. Kwa hivyo Jibril anampenda, kisha ananadi kwa wakazi wa mbinguni: Hakika Mwenyezi Mungu anampenda fulani, kwa hivyo mpendeni, basi na watu mpendeni, kwa hivyo, wanampenda wakazi wa mbinguni, kisha akaandikiwa kukubaliwa duniani." Na Mwenyezi Mungu aliwafanyia mapenzi, kwa sababu walimuenzi na kumpenda, kwa hivyo akawafanya kupendwa na walio karibu zaidi naye, vipenzi wake.