مريم
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يَوْمَ نَحْشُرُ ٱلْمُتَّقِينَ إِلَى ٱلرَّحْمَـٰنِ وَفْدًا ٨٥
{85} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu tofauti iliyoko kati ya makundi haya mawili: wachamungu na wahalifu. Na kwamba wale wanaomcha Yeye kwa kujiepusha na ushirikina, uzushi na maasia, atawakusanya kwenye mahali pa kisimamo cha Qiyama kwa utukufu, heshima, na taadhima. Na kwamba marejeo yao ni Mwingi wa rehema, na makusudio yao ni Mwingi wa kutoa (Al-Mannan), kama wageni wake. Na mgeni lazima huwa moyoni mwake na matumaini na mawazo mazuri juu ya anayemuendea ugeni, kama inavyojulikana. Basi wachamungu watakwenda ugeni kwa Mwingi wa rehema, wakitaraji rehema yake na ihsani yake ya kujumuisha, na kufikia vipawa vyake katika nyumba ya radhi zake. Na hayo ni kwa sababu ya yale matendo waliyoyatanguliza kwa kumcha na kufuata yale anayoyaridhia, na kwamba Mwenyezi Mungu aliwaahidi thawabu hizo kwa ndimi za Mitume wake. Kwa hivyo wakaelekea kwa Mola wao Mlezi wakiwa wana utulivu juu ya hilo, wakiwa wana imani na fadhila zake.