مريم
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ثُمَّ لَنَنزِعَنَّ مِن كُلِّ شِيعَةٍ أَيُّهُمْ أَشَدُّ عَلَى ٱلرَّحْمَـٰنِ عِتِيًّا ٦٩
{69} Na ndiyo sababu akataja hukumu yake kuhusiana nao, akasema, "Kisha kwa yakini tutaondoa katika kila kundi wale miongoni mwao waliozidi kumuasi Arrahmani (Mwingi wa Rahema)." Yaani, kisha kwa yakini tutaondoa kutoka katika kila kundi miongoni mwa madhalimu, waliofanana katika dhuluma, ukafiri na uasi, wale wao waliozidi katika uasi, wenye dhuluma kubwa zaidi, wenye ukafiri mkubwa ili awatangulize kutiwa adhabu. Kisha hivyo hivyo atatangulizwa mwenye dhambi kubwa katika adhabu zaidi, kisha mwenye dhambi kubwa zaidi. Nao katika hali hiyo watalaaniana wao kwa wao, na wa mwisho wao atasema kuhusu wa mwanzo wao, "Mola wetu Mlezi! Hawa ndio waliotupoteza. Basi wape adhabu ya Motoni marudufu. [Atasema: Kila mmoja ana marudufu, lakini nyinyi hamjui tu]. Na wa mwanzo wao atamwambia wa mwisho wao: Basi nyinyi pia hamkuwa na ubora wowote kuliko sisi..."