مريم
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يَرِثُنِى وَيَرِثُ مِنْ ءَالِ يَعْقُوبَ ۖ وَٱجْعَلْهُ رَبِّ رَضِيًّا ٦
{6} Na urithi huu ni urithi wa kidini, utume, elimu na matendo, na ndiyo maana akasema, "Anirithi na awarithi ukoo wa Yaaqub. Na umjaalie ewe Mola wangu Mlezi awe mwenye kuridhisha." Yaani, mja mwema ambaye utamridhia na kumfanya kupendwa waja wako. Na jumla ya hayo ni kwamba alimwomba Mwenyezi Mungu ampe mwana mwema wa kiume ambaye atasalia baada ya kifo chake na awe msimamizi baada yake, na pia awe nabii aliyeridhiwa kwa Mwenyezi Mungu na kwa viumbe vyake. Na huyu ndiye mwana bora zaidi. Na katika rehema za Mwenyezi Mungu kwa mja wake ni kwamba amruzuku mwana mwema aliyekusanya tabia njema na sifa nzuri. Kwa hivyo Mola wake Mlezi akamrehemu na akaitikia dua yake, na akasema: