مريم
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يَـٰٓأُخْتَ هَـٰرُونَ مَا كَانَ أَبُوكِ ٱمْرَأَ سَوْءٍ وَمَا كَانَتْ أُمُّكِ بَغِيًّا ٢٨
{28} Inaonekana dhahiri katika kuali yake, "Ewe dada yake Harun" kwamba Harun huyu ni kaka yake Maryamu wa kweli, na ndiyo maana wakamnasibisha Maryamu naye. [Nao walikuwa wakiitana kwa majina ya Manabii, na huyu si Harun bin Imran, kakaye Musa, kwa sababu kuna vizazi vingi sana kati yao]. "Baba yako hakuwa mtu mbaya, wala mama yako hakuwa kahaba." Walikuwa watu wema waliosalimika na maovu, na hasa uovu huu ambao wanauashiria hapa. Nao wanamaanisha kwamba: Vipi umesifika na yale ambayo hawakusifika nayo wao, na ukafanya kitu ambacho hawakuwahi kukifanya? Na hilo ni kwa sababu kizazi mara nyingi wanatokana wao kwa wao kuhusiana na kutengenea na kinyume chake. Kwa hivyo wakastaajabu sana kulingana na yale yaliyothibiti katika nyoyo zao. Vipi akafanya hilo?