انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الكهف
السورة ١٨

الكهف

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٩٤

قَالُوا۟ يَـٰذَا ٱلْقَرْنَيْنِ إِنَّ يَأْجُوجَ وَمَأْجُوجَ مُفْسِدُونَ فِى ٱلْأَرْضِ فَهَلْ نَجْعَلُ لَكَ خَرْجًا عَلَىٰٓ أَن تَجْعَلَ بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمْ سَدًّا ٩٤

{94} Mwenyezi Mungu alimpa Dhul-Qarnain njia za kielimu ambazo kwazo aliweza kufahamu lugha za kaumu wale na ufahamu wao wa kisheria, na akawaongea na wao, nao wakamuongelesha. Kwa hivyo, wakamlalamikia kuhusu madhara yaliyofanywa na Yaajuju na Maajuju, ambao walikuwa umma mbili kubwa kubwa za wanadamu. Wakasema, "Hakika Yaajuju na Maajuju wanafanya uharibifu katika ardhi" kwa kuua na kuchukua mali na mengineyo. "Basi je, tukupe ujira ili utie baina yetu na baina yao kizuizi?" Na hilo lilionyesha kwamba wao wenyewe hawakuweza kukijenga kizuizi hicho, na wakajua uwezo wa Dhul-Qarnain wa kufanya hivyo. Kwa hivyo wakampa malipo ili afanye hivyo, na wakamtajia sababu ya hilo, ambayo ni uharibifu wao (Yaajuju na Maajuju) katika ardhi.