الكهف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَدَخَلَ جَنَّتَهُۥ وَهُوَ ظَالِمٌ لِّنَفْسِهِۦ قَالَ مَآ أَظُنُّ أَن تَبِيدَ هَـٰذِهِۦٓ أَبَدًا ٣٥ وَمَآ أَظُنُّ ٱلسَّاعَةَ قَآئِمَةً وَلَئِن رُّدِدتُّ إِلَىٰ رَبِّى لَأَجِدَنَّ خَيْرًا مِّنْهَا مُنقَلَبًا ٣٦
{35 - 36} Kisha hakukumtosha kujifahiri kwake huku mbele ya mwenzake mpaka akahukumu kwa ujinga wake na dhuluma yake, na akafikiri alipoingia kitaluni mwake, "Akasema: Sidhani kabisa kuwa haya yatawahi haribika milele.” Basi akawa na utulivu juu ya dunia hii na akairidhia, na akakanusha kufufuliwa, na akasema, “Wala sidhani kuwa hiyo Saa (ya Qiyama) itatokea. Na ikiwa" kwa mfano "nitarudishwa kwa Mola wangu Mlezi, bila ya shaka nitapata marejeo bora zaidi kuliko haya." Yaani, atanipa kilicho bora zaidi kuliko vitalu hivi viwili! Na hili halikosi kuwa na mambo mawili: Ima yeye anajua uhakika wa hali yake ya akhera, kwa hivyo yakawa maneno yake hayo ni kwa njia ya kejeli na masihara, kwa hivyo hilo likawa ni kuongeza ukafiri juu ya ukafiri wake. Au awe anadhani tu kuhusu uhakika huo, kwa hivyo akawa ni katika watu wajinga zaidi wasiokuwa na akili hata kidogo. Kwa maana, kuna uwiano gani baina ya kipawa cha duniani na kipawa cha akhera, mpaka anafikiri kwa ujinga wake kwamba anayepewa duniani atapewa akhera? Bali, uwezekano mkubwa zaidi ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu huwakunjia dunia vipenzi wake na wateule wake, na awakunjulia dunia maadui wake, ambao hawana fungu lolote katika Akhera. Na la dhahiri ni kuwa anajua uhakika wa hali hiyo, lakini akasema maneno haya kwa kejeli na masihara, kwa ushahidi wa kauli yake, "huku anajidhulumu nafsi yake" kwa maana, kuthibitisha kuwa yeye anasifika kwa sifa ya dhuluma katika kuingia kwake, kama alivyosema alichosema, inaonyesha uasi wake na ukaidi wake.