الكهف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَٱضْرِبْ لَهُم مَّثَلًا رَّجُلَيْنِ جَعَلْنَا لِأَحَدِهِمَا جَنَّتَيْنِ مِنْ أَعْنَـٰبٍ وَحَفَفْنَـٰهُمَا بِنَخْلٍ وَجَعَلْنَا بَيْنَهُمَا زَرْعًا ٣٢
{32} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake- rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: - Wapigie watu mfano wa wanaume hawa wawili: mwenye kushukuru neema ya Mwenyezi Mungu, na mwenye kuikufuru, na maneno na matendo ambayo kila mmoja wao alifanya, na adhabu na thawabu za haraka na za baadaye zilizotokea kwa sababu ya hayo, ili wazingatie kutokana na hali zao hizo, na waaidhike kutokana na yaliyowapata. Na hakuna faida yoyote wala matokeo yenye manufaa katika kujua wanaume hao wawili walikuwa ni akina nani na walikuwa katika wakati gani au mahali gani. Matokeo mazuri yanapatikana tu kutoka katika kisa chao, na kutafuta yasiyokuwa hayo, ni katika kujisumbua bure. Basi mmoja wa wanaume hawa wawili aliyekufuru neema kubwa ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu alimfanyia vitalu viwili vizuri "vya mizabibu, na tukavizungushia mitende." Nayo mizabibu ikawa iko katikati yake, kwa hivyo vikawa na sura nzuri ya kuvutia, na miti na mitende yake ikainuka juu kiwango cha kuangazwa na jua na kufikiwa na upepo, mambo ambayo kwayo matunda hukomaa na kuiva. Licha ya hayo, aliweka mazao kati ya miti hiyo.