الكهف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ٱلَّذِينَ كَانَتْ أَعْيُنُهُمْ فِى غِطَآءٍ عَن ذِكْرِى وَكَانُوا۟ لَا يَسْتَطِيعُونَ سَمْعًا ١٠١
{101} Na hizi ndizo athari za matendo yao na malipo ya vitendo vyao. Kwa maana, wao katika dunia hii, macho yao yalikuwa yamefunikwa kutokana na kumkumbuka Mwenyezi Mungu, wakawa wamelipa mgongo jambo la kumkumbuka Mwenyezi Mungu, Mwenye hekima, na Qur-ani Tukufu. ''Na wakasema: nyoyo zetu ziko katika vifuniko kwa yale unayotuitia.'' Na machoni mwao kuna vizibo vinavyowazuia kuona ishara za Mwenyezi Mungu zenye manufaa. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na kwenye macho yao kuna vifuniko.'' "Na wakawa hawawezi kusikia" ishara za Mwenyezi Mungu zinazofikisha katika Imani; kwa kuwa waliichukia Qur-ani na Mtume. Kwa maana, mwenye kuchukia hawezi kuyapa masikio yake maneno ya yule ambaye yeye anamchukia. Kwa hivyo, zinapozuilika njia za kupata elimu na heri, basi hawana uwezo wa kusikia wala kuona wala hawana akili yenye kunufaisha. Kwa kuwa walimkufuru Mwenyezi Mungu, na wakazikataa Ishara zake, na wakawakadhibisha Mitume wake, basi wakastahiki Jahannam, na hayo ndiyo maishio mabaya mno.