الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَمِنَ ٱلَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِۦ نَافِلَةً لَّكَ عَسَىٰٓ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا ٧٩
{79} Na kauli yake, "Na amka usiku kwa ibada." Yaani, swali katika wakati wake wowote. "Ni ziada ya sunna hasa kwako wewe," ili swala hii ya usiku ikuzidishie utukufu na kunyanyuliwa daraja. Tofauti na wengine, hiyo kwao itakuwa ni kafara ya matendo yao mabaya. Na inawezekana kwamba maana yake ni kwamba swala tano za kila siku ni wajibu kwako na kwa Waumini. Tofauti na swala ya usiku, hiyo ni wajibu kwako tu hasa. Kwa sababu ya utukufu wako mbele ya Mwenyezi Mungu, akaufanya wajibu wako kuwa mkubwa zaidi kuliko wengine, na ili malipo yako yawe mengi, kwa hivyo upate nafasi ya kusifiwa, ambayo ni nafasi ambayo watamsifu kwayo watu wa mwanzo na wa mwisho. Nafasi ya uombezi mkubwa, wakati viumbe vitakapoomba kuombewa msamaha na Adam, kisha Nuhu, kisha Ibrahim, kisha Musa na Isa, na wote watatoa udhuru wa kutoweza kufanya hivyo na asifanye hivyo, mpaka watakapoomba uombezi kwa bwana wa wana wa Adam ambaye ni yeye mtume Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ili Mwenyezi Mungu awarehemu kutokana na wasiwasi kubwa na dhiki ya hali ngumu watakayokuwamo. Kisha atawafanyia uombezi kwa Mola wake Mlezi, naye atakubaliwa uombezi wake na atamsimamisha mahali ambapo wa mwanzo na wa mwisho watamuonea gere, na atakuwa amewasababishia viumbe wote kupata neema kubwa sana.