الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَفَأَمِنتُمْ أَن يَخْسِفَ بِكُمْ جَانِبَ ٱلْبَرِّ أَوْ يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ثُمَّ لَا تَجِدُوا۟ لَكُمْ وَكِيلًا ٦٨ أَمْ أَمِنتُمْ أَن يُعِيدَكُمْ فِيهِ تَارَةً أُخْرَىٰ فَيُرْسِلَ عَلَيْكُمْ قَاصِفًا مِّنَ ٱلرِّيحِ فَيُغْرِقَكُم بِمَا كَفَرْتُمْ ۙ ثُمَّ لَا تَجِدُوا۟ لَكُمْ عَلَيْنَا بِهِۦ تَبِيعًا ٦٩
{68 - 69} Na kwa sababu hii, Mwenyezi Mungu akawakumbusha kwa kauli yake, "Je, mna amani ya kuwa hatawadidimisha upande wowote katika nchi kavu, au kwamba hatawatumia tufani la kokoto?" Kwa maana Yeye ni Muweza juu ya kila kitu. Akitaka, atawateremshia adhabu kutokea chini yenu kwa kuwadidimiza, au kutokea juu yenu kwa tufani la kokoto na iwaache wameangamia. Basi msidhani kwamba kuangamia hakutokei isipokuwa baharini. Na ikiwa mnadhani hivyo, basi kwani mna amani kuwa, "Hatawarudisha" baharini "mara nyingine na akawatumia kimbunga cha upepo." Yaani, upepo mkali sana utakaoharibu chochote unachokifikia, "akawazamisha kwa mlivyokufuru, na kisha msipate wa kuwanusuru kutokana nasi." Kwa maana Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu hata uzito wa chembe.